"Imetuwia vigumu
watu wa hii kaumu
Kukutana kwa misimu
Na mengi tunayoka!"
NAAM kama utenzi huu mfupi unavyoashiria sikuhizi ni muhali kwetu sisi kukutana na kupeana maawazo.
Basi kutokana na sababu hii na mimi ninajiunga na waanzishaji blogi nyingine ili angalau wale wanaojali uhai wangu na mawazo yangu tuweze kuwasiliana.
Kweli fimbo ya mbali haiuwi nyoka, lakini blogi ni nusu ya kujuliana hali. Karibuni!
Na pengine zaidi hupatikana kwa mfano kujua kinachoendelea, kupiga umbeya na kuwatia wanaojilimbikizia kwa kufuru uoga na aibu wapipato mitaani!
Friday, November 16, 2007
Subscribe to:
Posts (Atom)
