MBONA mimi siwaelewi hawa Wazungu! Eti wanasema hakuna kazi. Ajira sasa ni ngumu? Hivi ni kweli ? Ninavyoona mimi ni kuwa jamaa hawa wanaonesha tu ubinafsi jambo ambalo kwa kawaida wamelizoea. Ajira zipo tena kabakaba. Hebu jiulize:
. Hakuna barabara na madaraja ya kujenga Afrika ?
. Waafrika wangapi wanaishi katika nyumba zinazostahili kuitwa nyumba ?
. Je tuna madaktari wa kutosha Afrika ?
. Je, tuna walimu wa kutosha Afrika ?
. Je asilimia ngapi ya watu wetu wanapata umeme na maji safi ? Ongeza na maswali mengine kiasi utakacho na majibu utakayopata ni kwamba ajira kwa wazungu wote wasio na ajira na wanaotaka kuja kufanya kazi ili kuijenga Afrika zipo. Tatizo ni ubinafsi wa Viongozi wao ambao wanasema heri wawalipe watu wao mshahara bila kufanya kazi kuliko waje kuijenga Afrika ? Na hicho wanacholipwa hivi kweli hakijaibiwa na wachimba dhahabu na almasi na madini mengine watokao Marekani, Canada na Australia ?
Ajira ipo, ila ubinadamu na utu hamna!
Thursday, May 28, 2009
Monday, May 25, 2009
Baada ya Mbagala kifanyike nini ?
Kila kitu na mahala pake na wakati wake. Miaka ya leo sio ya jana. Na watu wa leo hawana subira wala hadhari kama waliowatangulia. Kwa hiyo sioni sababu ya ubishi juu ya nini kifanyike baada ya baa la mabomu ya Mbagala.
Makambi ya jeshi na maghala mengine yenye zana na vifaa hatari lazima vikae mbali na watu. Kwa Dar es salaam na miji mingine hii ina maana makambi hayo yawe ni miji mbali na mji. Ndivyo wenzetu wanavyofanya. Kila kambi ya jeshi inakuwa sio chini ya kilomita 100 toka mjini au mwendo wa masaa mawili kwa taratibu toka mji wa raia wa karibu. Na katikati ya miji hii ya kijeshi na miji ya raia kunakuwa na msitu uliozunguka miji hiyo na maeneo yasiyoruhusiwa mtu kujenga au kufanya shughuli nyingine yoyote ya kijamii na kiuchumi.
Tuamke ili twende na wakati hapana kwa kweli sababu ya ubishi wowote. Kuna gharama zake. Lakini nini kilicho na bei kuliko roho ya Mtanzania?

Subscribe to:
Posts (Atom)