Kila kitu na mahala pake na wakati wake. Miaka ya leo sio ya jana. Na watu wa leo hawana subira wala hadhari kama waliowatangulia. Kwa hiyo sioni sababu ya ubishi juu ya nini kifanyike baada ya baa la mabomu ya Mbagala.
Makambi ya jeshi na maghala mengine yenye zana na vifaa hatari lazima vikae mbali na watu. Kwa Dar es salaam na miji mingine hii ina maana makambi hayo yawe ni miji mbali na mji. Ndivyo wenzetu wanavyofanya. Kila kambi ya jeshi inakuwa sio chini ya kilomita 100 toka mjini au mwendo wa masaa mawili kwa taratibu toka mji wa raia wa karibu. Na katikati ya miji hii ya kijeshi na miji ya raia kunakuwa na msitu uliozunguka miji hiyo na maeneo yasiyoruhusiwa mtu kujenga au kufanya shughuli nyingine yoyote ya kijamii na kiuchumi.
Tuamke ili twende na wakati hapana kwa kweli sababu ya ubishi wowote. Kuna gharama zake. Lakini nini kilicho na bei kuliko roho ya Mtanzania?
Monday, May 25, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment